SERIKALI
imetangaza kuzichukulia hatua kali za kinidhamu ikiwepo kuzifutia
usajili shule binafsi zitakazowafukuza au kuwakaririsha wanafunzi wa
kidato cha pili ambao hawatafikia wastani wa alama zilizowekwa na shule
husika.
Kauli hiyo ilitolewa
bungeni mjini Dodoma jana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Dkt.Shukuru Kawambwa, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum
(CHADEMA) Conchestar Lwamulaza, kuhusu malalamiko ya wamiliki kuweka
alama za juu za ufaulu kwa wanafunzi wa kidato cha pili.
Alisema walipokea
malalamiko mbalimbali ya wazazi juu ya suala hilo na kwamba Serikali
inakataza kutokumkaririsha darasa, kumhamisha wala kumfukuza kwani
tayari Serikali kupitia kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo alishaandika
barua kwenda kwa wamiliki wa shule na mameneja kuhusiana na jambo hilo.
Alisema waraka wa 10 wa mwaka 2012 wa elimu unazuia kumfukuza mwanafunzi akiwa mwaka wa mwisho wa masomo.
Dkt. Kawambwa alisema
baada ya kupokea malalamiko mbalimbali ya wazazi, Serikali inapiga
marufuku suala hilo kwani wastani wa kufaulu kwa mwanafunzi wa kidato
cha pili ni alama 30.
"Natoa agizo mbele ya
Bunge lako Tukufu kuwa kwa wamiliki na mameneja wa shule zisizokuwa za
Serikali kuanzia sasa yeyote atakayekaidi agizo hilo atachukuliwa hatua
kali za kisheria," alisema Dkt.Kawabwa.
Katika hatua nyingine;
Dkt. Kawambwa alisema Serikali inaendelea kijipanga ili kutekeleza agizo
la Rais Jakaya Kikwete kuwa mwaka 2016 shule zote za msingi na
Sekondari wanafunzi watasoma bure bila kulipa.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment