Akizungumza katika bunge hilo Mbatia amesema kuwa
kitendo cha polisi cha kuwapiga raia wasiokuwa na hatia, kuwazalilisha
waandishi wa habari na kupiga mabomu ya machozi kiasi cha kuwafanya
watoto wadogo kuhangaika hakikubaliki.
Amesema polisi wakiendelea kuachwa kufanya vitu
vya uvunjifu wa Amani Serikali haitatawalika hivyo ili kurejesha amani
na imani ya wananchi kwa Serikali yao ni vema shughuli zote za Bunge
zikaahirishwa kupisha mjadala wa hoja hiyo binafsi kwa lengo la
kuinusuru nchi.
“Mheshimiwa Spika naliomba bunge lako liahirishe
shughuli zake ili leo tuweze kujadili suala hili la uvunjifu wa amani
uliofanywa na jeshi letu la polisi jijini Dar es Salam jana, wao
wanasema kuwa wamepewa amri kutoka ngazi za juu tunataka serikali
ituambie ni nani anayetoa amri hizi za kupiga watu wasiokuwa na hatia
yeyote, amesema Mbatia.
Baada ya kuwasilisha hoja hiyo asilimia kubwa ya
wabunge walisimama juu Kisha kuunga mkono hoja hiyo lakini Spika
Makinda akawaomba wakae ili aweze kutoa ufafanuzi kwa mujibu wa kanuni.
Spika makinda aliwaeleza wabunge hao kuwa suala
hilo ni nyeti kwa sababu ni la kiusalama, ili kupata ufafanuzi zaidi
anaiagiza Serikali kufikisha bungeni hapo majibu ya hoja hiyo kesho ili
wabunge waweze kujadili.
Baada ya maamuzi hayo ya Spika Makinda kelele
zikasikika bungeni huku wabunge wakitaka kufanyika kwa mjadala huo leo
leo, ndipo Spika alipoamua kuahirisha bunge hadi saa kumi jioni.
0 comments:
Post a Comment