HOFU YATANDA TANZANIA:Uandikishwaji daftari la wapiga kura wasogezwa!!

Nembo ya Tume ya Uchaguzi Tanzania, chini yake ni mwanamke mmoja akimsaidia mwenzake kumwonyesha sehemu ya kupiga kura. Picha na Maktaba.
Tume ya uchaguzi nchini Tanzania imesogeza mbele kwa wiki moja zaidi tarehe ya kuzinduliwa kwa zoezi la daftari la wapiga kura litakalotumia mfumo mpya wa kieletroniki yaani Biometric Voters Registration BVR.

 Zoezi hilo ambalo litaanza rasmi katika mkoa wa Njombe na baadae kufuatia katika mikoa mengine ya Tanzania hivi sasa linatarajiwa kuanza tarehe 23 ya mwezi huu badala ya tarehe 16 kama ilivyokuwa imepangwa hapo awali.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini humo amesema lengo la mabadiliko hayo ni kuvipa fursa vyama vya kisiasa kujiandaa na kuandaa watu wake. Hata hivyo baadhi ya viongozi wa vyama vikuu vya kisiasa wamesema kauli hiyo haina ukweli wowote na kwamba tume inajikosha kwa sababu haina vifaa vya kutosha vya kuendesha uandikishaji huo.

 Wakati ikiwa imesalia miezi miwili tu na wiki kadhaa kabla ya tarehe iliyopangwa ya kupiga kura ya maoni ya katiba inayopendekezwa, wasi wasi unazidi kutanda miongoni mwa viongozi mbali mbali wa vyama vya kisiasa hapa nchini Tanzania, iwapo Tume ya Uchaguzi nchini humu itaweza kuboresha daftari la wapiga kura katika kipindi cha muda mfupi uliobakia.

 Baadhi ya viongozi hao wamesema kwamba licha ya tume hiyo kutovishirikisha vyama vya kisiasa katika baadhi ya maamuzi yake, lakini pia wamebaini kwamba mpaka sasa tume hiyo inakabiliwa na ukosefu wa vifaa vya uandikishaji kwa sababu havijaingia nchini kama ambavyo anabainisha Freeman Mbowe mwenyekiti wa Chadema.

Mfumo huu mpya kwa Tanzania wa BVR utaigharimu tume kiasi cha fedha za kitanzania shilingi bilioni mia mbili na tisini na tatu ambazo mpaka sasa haijafahamika iwapo fedha hizo zimepatikana au la. 

Kwa upande wake, Prof. Ibrahim Lipumba ambae ni mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF anaelezea kuwa kukosekana kwa utaalam miongoni mwa wafanyakazi wa tume kunaweza kuwa kikwazo cha kufanikisha zoezi hilo.

Hata hivyo, Jaji Damian Lubuva ambaye ndiye mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Tanzania anasema madai hayo ni uoga wa wanasiasa ambao hawataki mabadiliko katika mifumo ya uchaguzi.

Uandikishaji wapigakura umepangwa kufanyika nchi nzima kwa muda wa siku sitini kuanzia mkoani Njombe tarehe 23 mwezi huu ambapo watanzania zaidi ya milioni 23 wanatarajiwa kujitokeza katika uandikishaji huo.

 Hata hivyo kwa mujibu wa wachambuzi wa mambo, haijafahamika iwapo raia wengi watajitokeza kwa sababu kazi ya kuwahamasisha raia bado haijafanyika na vile vile baadhi ya watanzania wanaweza kuikosa fursa hiyo ikizingatiwa ni msimu wa wakulima kuingia mashambani kabla ya mvua za masika.

NEC, Vyama vya siasa wakutana kujadili maboresho daftari la wapiga kura

Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva akitoa taarifa kwenye mkutano na vyama vya siasa.
Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva akitoa taarifa kwenye mkutano na vyama vya siasa.
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe (kulia) na katibu mkuu wa Chadema Wilbroad Slaa katika mkutano na    Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe (kulia) na katibu mkuu wa Chadema Wilbroad Slaa katika mkutano na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba.
Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba.
Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye(kushoto)
Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye(kushoto).

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)  leo   imekutana  na viongozi wa vyama siasa jijini Dar es salaam.Katika mkutano huo Tume ya Taifa imetoa tathimini ya zoezi la majaribio  la Uboreshwaji wa Daftari la Kudumu  la Wapigaji kura katika majimbo ya  majaribio.

Aidha, majimbo ya majaribio ambayo tume ya Taifa ya Uchaguzi imeandikisha kwa kutumia teknolojia ya Biometric Voter Registration  (BVR) ni  Kawe, Dare s salaam, Kilombero Morogoro, pamoja  na  Milele mkoani Katavi.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Tume, Julias Maluba amesema kuwa maandalizi mengine waliyofanya ni pamoja na uhakiki wa vituo vya kuandikishia wapiga kura, katika ngazi ya vitongoji, vijiji na mitaa, hivyo tume imefanikiwa kuongeza vituo vingine vipya kutoka vituo 24,919 hadi vituo 36,109 vya sasa.

Akizungumzia  changamoto Malaba amesema kuwa ni pamoja na ‘setting’ za mashine inayotumika katika zoezi hilo la uchukuaji wa alama za vidole na  majina ya wenye alama.

Mkutano huo umejiri kufuatia vyama vya upinzani kuilaumu tume hiyo kwa kutowashirikisha kama ambavyo waliahidiwa na tume hiyo kabla ya kuanza zoezi la uandikishaji.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment