|  | 
| Rais Goodluck Johnathan wa Nigeria | 
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan 
amekana kwamba alishauriwa kuhusu kuahirisha  uchaguzi wa Urais 
nchini humo siku ya jumamosi.
Kucheleweshwa kwa uchaguzi kwa kipindi cha wiki moja sio kitu kikubwa alisema katika runinga ya taifa hilo la Nigeria.
Upinzani unadai kwamba bwana Johnathan alilazimisha uchaguzi huo kucheleweshwa kwa kuwa alikuwa anaogopa kushindwa.
Uchaguzi huo umeahirishwa hadi 28 mwezi machi.
Wachanganuzi wanasema kuwa uchaguzi huo ndio ulio na ushindani mkali tangu uongozi wa kijeshi ulioisha mwaka 1999.
0 comments:
Post a Comment