Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene. |
Akizungumza baada ya mkutano wa pamoja kati ya wadau na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene amezitaka taasisi hizo kuangalia uwezekano wa kushusha gharama za umeme ili kushuka kwa mafuta kuwaguse moja kwa moja wananchi wa kawaida.
Aidha, Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) nayo imetakiwa kuangalia namna itakavyoweza kushusha bei za nauli ili kushuka kwa gharama za mafuta ziendane na unafuu wa maisha kwa wananchi wote.
Waziri Simbachawene ameiomba Sumatra iweze kuchukua hatua za haraka za kutangaza bei mpya za nauli ambazo zitakuwa chini tofauti na ilivyo sasa.
Kwa upande mwingine bei ya bidhaa za petroli zimekuwa zikishuka bei kutokana na kushuka kwa bei katika soko la dunia ambapo unafuu umeanza kuonekana kwa watumiaji mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa.
0 comments:
Post a Comment