Mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya
kupambana na maswala ya rushwa katika umoja wa Africa kutoka Ghana
Mh.Daniel Batidam akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo
mbalimbali vya habari jijini Arusha katika ukumbi wa mikutano AICC
katika kuangalia jinsi gani wataweza kupambana na kufikia malengo ya
kutokomeza Rushwa ndani ya Bara La Africa.(Habari picha na Pamela Mollel
wa jamiiblog)
Makamu Mwenyekiti bodi ya ushauri ya kupambana na maswala ya rushwa katika umoja wa Africa Mh.Florince Ziyambi kutoka Zimbabwe
Muongoza vikao kutoka Kenya Mh.John Tuta akitambulisha wajumbe
Mwaandishi wa habari Merry Mwita akiuliza maswali katika mkutano huo
Muonekano ndani ya ukumbi
Picha ya Pamoja ya
Wakuu wa taasisi za kuzuia Ruswa
barani Africa
Wakuu wa taasisi za kuzuia Ruswa
barani Africa wamekutana katika ukumbi wa mikutano AICC katika
kuangalia jinsi gani wataweza kupambana na kufikia malengo ya kutokomeza
Rushwa ndani ya Bara La Africa.
Wakuu hao ambao ni wajumbe wa
Bodi ya Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa barani Afrika AUABC
iliyopo chini ya jumuia ya muungano wa nchi za Afrika ambapo mwenyekiti
wa Taasisi ya AUABC Jaji Daniel Batidam amesema kuwa wanatarajia kwa
mkutano huu utasaidi kupunguza makali ya Ruswa ndani ya bara hili.
Amesema kuwa kiwango kikubwa
wanaangalia jinsi gani wataweza kuondoa ruswa katika taasisi za jamii
kwa maana ndio zinazochangia kwa kiasi kikubwa maenbdeleo ya nchi zetu
za kiafrika.
Pamoja na hayo amesema kuwa
tatizo kubwa la Rushwa ndani ya bara la Afrika ni mfumo uliopo ambao
unakuwa unaweka mianya ya rushwa pamoja na hayo alisisistiza kwa
wananchi kuacha kutoa rushwa ili kuiondoa kabisa.
Bodi hiyo imeundwa na watu 11 kutoka nchi mbalimbali barani Africa
0 comments:
Post a Comment