Siku moja baada ya sakata la waandishi wa
habari kupokea kipigo wakati wakiwa eneo la kazi makao makuu ya polisi jana,jukwaa la
wahariri Tanzania(TEF) limeibuka na tamko zito la kulaani kitendo hicho kwa
kile walichodai kuwa ni mwendelezo wa kuendelea kuwaadabisha wanahabari wakati
wakitekeleza majukumu yao.
Hayo yamesemwa Jijini Dar Es Salaam na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri nchini (TEF)Absalom
Kibanda wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari ambapo Kibanda alisemwa wao
Jukwaa la Wahariri wamesikitishwa na kitendo cha Kinyama walichofanyiwa Waandishi
wa habari wakati wakitekeleza majukumu yao ya kawaida.
“sisi kama jukwaa la wahariri tumesikitika sana kwa
kitendo cha jana na huu ni mwendelezo wa matukio ya kutembeza vipigo kwa
wanahabari wakati wakiwa katika maeneo yao ya kazi”alisema kibanda.
Aidha
jukwaa hilo limewataka jeshi la polisi kufanya mambo kadhaa kabla ya jukwaa
hilo halijachukua hatua zaidi ambapo kati ya mambo hayo ni pamoja na kuwakamata
mara moja askari watatu ambao wanaonekana katika picha wakimshambulia mwandishi
wa gazeti la Tanzania daima Josephat isango.
Pia wamelitaka jeshi la polisi kufanya ukaguzi wa elimu na uwezo wa askari wao kwa kile alichosema kuwa kama askari anatambua majukumu yake ya kazi hawezi kufanya kitendo cha kinyama kama kile cha jana kwa wanahabari hivyo wanamtaka mkuu wa jeshi la polisi kuhakikisha wanafanya usafi kwa askaria ambao hawana sifa ndani ya jeshi hilo.
Katika tukio la jana jeshi la polisi kwa kupitia askari wake walijikuta
wakiwashambulia wanahabari bila kujulikana sababu mara moja ambapo wanahabari kadhaa walijeruliwa.
0 comments:
Post a Comment